Vunjika mbavu
Wednesday, July 25, 2012
Vunjika mbavu: Mzazi huyu...........
Www.michuziblogspot.com
Sunday, April 15, 2012
Mzazi huyu...........
MTOTO: Baba ntumie hela ya matumizi huku shuleni hali ni mbaya la sivyo ntajinyonga.
BABA:huku nyumbani hali ni mbaya kuliko huko shuleni kwahiyo kama unajinyonga sawa tu kwa sababu utapunguza bajeti. Kopa kamba dukani nitakuja kulipa nitakapokuja kuchukuwa mwili. Mungu akulaze mahali pema peponi
Kuwa na Msimamo
Katika Daladala mama mmoja alitaka kumnyonyesha . Mtoto akakataa! Mama akamwambia "NYONYA KAMA HUTAKI NAMPA ANKO" (Anko ni kaka mmoja abiria aliekaa na huyo Mama pembeni) mtoto akanyonya kidogo na akaacha! Mama akamtishia tena kumpa Anko, ndipo yule kaka kwa hamaki akasema,; "MAMA UWE NA MSIMAMO, UNAJUA NIMEPITILIZA VITUO VINNE KWA AJILI YAKO, HEBU KUWA MKWELI! UNANIPA AU NISHUKE!?
Monday, January 30, 2012
Mwili mmoja
mume anaingia ndani kutoka kazini na kusema."mke wangu nina matatizo makubwa"
"sema tuna matatizo mume wangu sisi tu mwili mmoja" mke anapoza
"ok! tuna matatizo mke wangu, tumempa mimba secretary wetu" mume anasema.
Wednesday, January 11, 2012
Majambazi hawa nomaaaaa!
Jamaa mpenda wake za watu. siku moja alikuwa akila uroda na mke wa
jirani mtaa wa pili usiku wakati mumewe hayupo. Ghafla, mume karudi na
kuanza kupigahodi mlango wa mbele. mke kusikia mumewe karudi, kahamaki
na kukimbilia kumtoa jamaa kupitia mlango wa nyuma.
Jamaa alikurupuka mbio, akaruka ukuta akiwa uchi wa mnyama,akakimbia
hadi nyumbani kwake. Alipofika kwa mkewe, akamwambia kapigwa na
majambazi njiani wakamvua nguo zote na kumwibia kila kitu. Mkewe
akamwambia "Pole mpenzi lakini hawa majambazi si watu wema kabisa,yaani
wamekuvua nguo zote na kukuvalisha Condom!
nomaaaaaaaaaaaaaaa,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, ,,,
Ndoto
Jamaa 1 alikuwa kila siku anaota panya wanacheza mpira akaenda kwa mganga...ili aziondoe hizo ndoto.Mganga akampa dawa ambayo alitakiwa anywe leo kama sharti ili ndoto ziishe.
Jamaa akamwambia mganga mi sinywi leo ntakunywa kesho...alipo ulizwa kwanini akamwambia leo ndio fainali.
Haya makanisa sasa.....
Jamani hapa duniani kuna watu wana mambo ya ajabu, juzi nikiwa kanisani nilikaa karibu na kijana mmoja. Kijana huyu badala ya kusikiliza mahubiri yaliyokuwa yanatolewa na Padri pale kanisani akachukua sigara yake akawa anavuta pale pale alipoketi. Kwa kweli nilishituka nikataka kudondosha chupa yangu ya bia. Nilishangaa sana.
Subscribe to:
Comments (Atom)