Sunday, April 15, 2012

Mzazi huyu...........

MTOTO: Baba ntumie hela ya matumizi huku shuleni hali ni mbaya la sivyo ntajinyonga. BABA:huku nyumbani hali ni mbaya kuliko huko shuleni kwahiyo kama unajinyonga sawa tu kwa sababu utapunguza bajeti. Kopa kamba dukani nitakuja kulipa nitakapokuja kuchukuwa mwili. Mungu akulaze mahali pema peponi

Kuwa na Msimamo

Katika Daladala mama mmoja alitaka kumnyonyesha . Mtoto akakataa! Mama akamwambia "NYONYA KAMA HUTAKI NAMPA ANKO" (Anko ni kaka mmoja abiria aliekaa na huyo Mama pembeni) mtoto akanyonya kidogo na akaacha! Mama akamtishia tena kumpa Anko, ndipo yule kaka kwa hamaki akasema,; "MAMA UWE NA MSIMAMO, UNAJUA NIMEPITILIZA VITUO VINNE KWA AJILI YAKO, HEBU KUWA MKWELI! UNANIPA AU NISHUKE!?

Monday, January 30, 2012

Mwili mmoja

mume anaingia ndani kutoka kazini na kusema."mke wangu nina matatizo makubwa" "sema tuna matatizo mume wangu sisi tu mwili mmoja" mke anapoza "ok! tuna matatizo mke wangu, tumempa mimba secretary wetu" mume anasema.

Wednesday, January 11, 2012

Majambazi hawa nomaaaaa!

Jamaa mpenda wake za watu. siku moja alikuwa akila uroda na mke wa jirani mtaa wa pili usiku wakati mumewe hayupo. Ghafla, mume karudi na kuanza kupigahodi mlango wa mbele. mke kusikia mumewe karudi, kahamaki na kukimbilia kumtoa jamaa kupitia mlango wa nyuma. Jamaa alikurupuka mbio, akaruka ukuta akiwa uchi wa mnyama,akakimbia hadi nyumbani kwake. Alipofika kwa mkewe, akamwambia kapigwa na majambazi njiani wakamvua nguo zote na kumwibia kila kitu. Mkewe akamwambia "Pole mpenzi lakini hawa majambazi si watu wema kabisa,yaani wamekuvua nguo zote na kukuvalisha Condom! nomaaaaaaaaaaaaaaa,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, ,,,

Ndoto

Jamaa 1 alikuwa kila siku anaota panya wanacheza mpira akaenda kwa mganga...ili aziondoe hizo ndoto.Mganga akampa dawa ambayo alitakiwa anywe leo kama sharti ili ndoto ziishe. Jamaa akamwambia mganga mi sinywi leo ntakunywa kesho...alipo ulizwa kwanini akamwambia leo ndio fainali.

Haya makanisa sasa.....

Jamani hapa duniani kuna watu wana mambo ya ajabu, juzi nikiwa kanisani nilikaa karibu na kijana mmoja. Kijana huyu badala ya kusikiliza mahubiri yaliyokuwa yanatolewa na Padri pale kanisani akachukua sigara yake akawa anavuta pale pale alipoketi. Kwa kweli nilishituka nikataka kudondosha chupa yangu ya bia. Nilishangaa sana.

Huyu beki tatu sooooooo!

House girl mmoja kutoka nyanda za juu kusini ,alitoa kali ya mwaka alipohojiwa na bosi wake kwanini toothpick zinaisha haraka nae akajibu: Bee wanaofuja huto tuvijiti ni hawo wanao maana wakitumia mara moja tu wanatupa lakini mimi nikichokonoleaga meno bee narudishaga humohumo kwenye kachupa kake. Aaaargh!!!!!!!!!

Monday, January 9, 2012

Panya yupi ni nomaaaaa!

Panya wa3 walikuwa wanatambiana nani mkali zaidi ya wenzake.. Panya wa 1: mimi hata mtego uwekweje,nategua tu! Panya wa 2: mimi hata maziwa yawe yamewekwa sumu,mi nakunywa tu! Panya wa 3: ye akaanza kuondoka. Wenzake wakamuuliza, "we vipi?" Akajibu, "Naenda kufunga ndoa na PAKA...!" Je,yupi noma?

Bi Kidude na wazungu

Bi kidude alikwenda katika show london akafikia katika hotel ya kifahari akiwa chumbani kwake alichungulia nje akawaona watoto wa kizungu wanaogelea kwenye swimming pool naye akakumbuka mambo ya jahazi akatoka nje kimya akaingia kupiga mbizi alipoibuka watoto wote walipiga kelele na kukimbia walipoulizwa kuna nini walijibu kwa pamoja.There's a crocodile inside the pool!

Huu ubairi sasa balaaa!

Mzee mmoja wa kichagga tajiri kwa jina la MDAWA alipata ajali mbaya sana ya gari. Alipoteza fahamu na kupelekwa KCMC huku matumaini ya kupona yakiwa yametoweka kabisa. Kutokana na juhudi za madaktari (pengine na Mungu wake) aliweza kupata fahamu baada ya wiki tatu. Muda wote huo familia yake ilikuwa iko karibu naye kusubiri litakalotokea. Mkewe na watoto wake watatu waliruhusiwa kuwa naye pale ICU (Intensive Care Unit) kwa zamu. Basi baada ya kupata fahamu nesi aliyekuwa anamhudumia alimwambia; NESI: Baba pole sana MZEE MDAWA: Unanipa pole kwani nini kimetokea? NESI: Baba ulipata ajali mbaya sana ya gari wiki tatu zilizopita. MZEE MDAWA: Kweli, Kari yangu itakuwa imepona? NESI: Hapana imeharibika kabisa Baba. MZEE MDAWA: Hai jamani FII EKIS (VX) yangu. Niliinunua kwa bei kubwa mno. Sasa nitapata wapi nyingine...aaaiiii aaaaaaiii aaaaaiiii! NESI: Baba usilie, hilo mbona ni kidogo? Unajua mkono wako wa kushoto umekatika kabisa? MZEE MDAWA: Mkono wa kushoto? Umekatika? Ule mkono niliovaa ile saa yangu ya bei mbaya? Yaani saa yangu nayo imekwenda? Aaaiiii....aiiii...aiiiii, jamani saa yangu. NESI: Baba acha kulia, utaumia zaidi MZEE MDAWA: Hapana mwanangu, kama kari yangu na saa fyote fimekwenda kwa nini roho isiniume? Hifyo fitu ni fya bei mbaya sana ati... NESI: Baba tulia, familia yako iko hapa wanataka kukupa pole. MZEE MDAWA: Iko hapa ee? Mama Sikola, uko hapa? MAMA: Ndiyo ! mume wangu, siwesi kukuacha mwenyewe. Pole sana mpenzi. Tunamshukuru mungu sasa unaongea. Yesu asifiwe sana! MZEE MDAWA: Sawa, Kodilafu uko hapa? GODLOVE: Ndiyo Mzee, siwezi kukuacha mwenyewe katika hali hii. Pole sana Baba. MZEE:Sikola, na wewe uko hapa? SKOLA: Ndiyo Baba, hatuthubutu kukaa mbali na wewe ukiwa katika hali hii baba. Ni hali ya kutisha sana. MZEE: Na huyu kitinda mimba wangu Ferenaisi, yuko hapa? Verynice: Niko hapa baba, nyumba yote iko hapa kukupa pole. MZEE: Basi nyie wote hamna akili hata mmoja. Yaani Mmekuja wote hapa, dukani kabaki nani leo? Yaani munanona kari yangu ni hiyo imepika msinga tayari na saa yangu ya bei mbaya imepotea badala ya kukaa dukani wote munaongosana kuja huku KMCC. Nyie ni wajinga wa mwisho kabisa.

kelele bwana.

Ilitokea ajali ya barabarani lakini kwa bahati nzuri abiria walipata mikwaruzo tu kidogo isipokuwa mmoja ambaye alifariki hapo hapo. Katika walioumia, mmoja aliyekwaruzika mguu na kutoka damu nyingi, alikuwa analia kwa kelele. Baada ya kuona kelele zimezidi, abiria mmoja alishindwa kustahamili na kumkabili yule majeruhi. "Wewe ha**thi nini? Kelele tu! Yo yo yo, uwii uwii uwii! Mwangalie mwenzako yule pale, amekufa na yuko kimya, wewe kwa kuumia mguu tu kelele hatuna amani. Pumbafff!!!"

Sharobaro jeshini...

Sharobaro kajiunga na jeshi la wananchi, wamekaa mstari kwaajiri ya kukaguliwa gwaride, Afande akamfuata sharobaro akamuuliza ww mbona ujishughulishi, sharobaro akamjibu, Yooh Afande sijazoea mabuti nimezoea SUPRA men!!!!

Sunday, January 8, 2012

Ukichacha

http://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=25091&d=1300107175
Mshkaji anapuliza bange lake barabarani,Khafla katokea MALAIKA. BANGI MAN; >Wewe nani MALAIKA>Mimi malaika(ISRAILI) natoa roho za watu. BANGI MAN>AHHHH!!! MI NILIDHANI POLISI BWANA

Kwa Babu Loliondooooo!

Baada ya watu kuleta fujo kugombea KIKOMBE, Babu aliamua kuwapanga kwa mistari. Msitari wa kwanza wenye kansa, walikuwa wachache. Mstari pili walipangwa wa kisukari, wakawa wengi. Mstari wa tatu akasema wajipange wenye Ukimwi, ukakosa watu kabisa. BABU akamwambia msaidizi wakeamwage ile dawa ya kutibu ukimwi. Watu wakapiga kelele sana wakasema: USIIMWAGEEEE, NA HIYO TUTAKUNYWA HIVYO HIVYOOOOOOOOO!!!!!!!!!

Nani ana dhambi hapa?

Askofu aliendesha harambee kuchangia ujenzi wa kanisa. Wakristo wakatoa Tshs. 75,050/= tu. Ghafla majambazi wakateka kanisa na kuamrisha kila mtu atoe alichonacho!!! Majambazi wakakusanya Tshs.8,945,800/= cash, kisha wakamkabithi Askofu ili aendeleze ujenzi wa kanisa. Je, majambazi wana dhambi au wakristo wanathawabu ??
mzee mmoja alichoshwa na habari za mtaani kwamba mwanaye hata umuulize swali jepesi kupita yote ni lazima atakosa !!! Siku moja akaamua kuandaa swali jepesi kupita kiasi ili amuulize mwanae mbele ya watu kufuta ile historia mbaya !!! Siku ya siku ikafika mbele ya umati mshua akamuita mwanae kisha akamuuliza swali lifuatalo..... mwanangu mtu mwenye umri wa miaka kati ya 18 hadi 35 huitwa KIJANA..... Je mtu mwenye umri kuanzia 36 hadi 50 ataitwa nani !..... Toto bila hata ya kufikili kwa sauti likajb ANAITWA KIJUZI !!!! Vp angekuwa mwanao ungemfanyaje !....

UTAFANYA NINI?

Utafanyaje? unapoingia chooni na kukuta mtu kanya pembeni ya choo muda mfupi tu uliopita, unafikiria na unaamua kuahirisha, unatoka. Mara mlangoni unapishana na msichana mrembo unayemtamani siku zote hapo kazini kwenu anataka kuingia chooni. Utafanyaje?

Vunjika mbavu: Uzuzu

Vunjika mbavu: Uzuzu: Ukimpenda mtu asiyekupenda ni sawa na kusubiria boti uwanja wa ndege......... be care!

Uzuzu

Ukimpenda mtu asiyekupenda ni sawa na kusubiria boti uwanja wa ndege......... be care!